255 YESU UNIONYESHE

1. Yesu unionyeshe Msalaba wako,
Kisima cha Golgotha Chenye kusafisha.


Msalaba wa Yesu, Nausifu sana.
Yesu, ’nilinde hapo Hata nikuone!


2. Hapo niliiona Neema ya ajabu,
Nuru toka Golgotha Ilifika kwangu.


3. Yesu, ’nilinde hapo, Unifahamishe
Kwamba ulizibeba Dhambi zangu zote!


4. Unilinde daima Penye msalaba,
Nikupende, Mwokozi, Sasa na milele!

Comments