270 SIMAMA FANYA VITA

1. Simama fanya vita, askari wa Yesu!
Tuinue bendera ya ushindi wake!
Yeye huyaongoza, majeshi yake huku,
Adui wote pia, Bwana awashinda.


2. Sikia baragumu, linalotuita!
Tuendelee mbele, lengo ni kushinda!
Tusiogope kamwe, hatari za vitani,
Pigana na adui, kwa nguvu za Mungu!


3. Simama fanya vita, kwa jina la Yesu!
Yafaa sisi sote, kumtegemea.
Na kwanza tuzivae, silaha zake Mungu!
Tukeshe siku zote , tuombe kwa bidii!


4. Shindano letu hapa, hima litakwisha,
Ndipo tutapumzika, baada ya vita.
Na kila mshindaji, atapokea taji,
Na utukufu mwingi, karibu na Mungu.

Comments