266 NATAKA NIMJUE YESU

1. Nataka nimjue Yesu, Na nizidi kumfahamu,
Nijue pendo lake na Wokovu wake kamili.


Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu,
Nijue pendo lake na Wokovu wake kamili.


2. Nataka nione Yesu, Na nizidi kusikia,
Anenapo kitabuni, Kujidhihirisha kwangu.


3. Nataka nifahamu na, Nizidi kupambanua,
Mapenzi yake nifanye, Yale yanayompendeza.


4. Nataka nikae naye, Kwa mazungumzo zaidi,
Nizidi kuwaonyesha, Wengine wokovu wake.

Comments