326 YESU UNIPENDAYE

1. Yesu unipendaye Kwako nakimbilia,
Ni wewe utoshaye Mwovu akinijia;
Yafiche ubavuni Mwako maisha yangu;
Nifi'she bandarini, Wokoe moyo wangu.


2. Ngome nyingine sina; Nategemea kwako,
Usinitupe Bwana, Nipe neema yako,
N'sha kukwamania, Mwenye kuniwezesha;
Shari wanikingia Vitani wanitosha.


3. Nakutaka Mpaji Vyote napata kwako;
Niwapo muhitaji, Utanijazi vyako;
Nao waangukao Wanyonge wape nguvu;
Poza wauguao, Uongoze vipofu.


4. Bwana umeniosha Moyo kwa damu yako;
Neema ya kutosha Yapatikana kwako;
Kwako Bwana naona Kisima cha uzima;
Mwangu moyoni, Bwana, Bubujika daima.


Comments