327 PELELEZA NDANI YANGU

1. Peleleza ndani yangu, Iwe safi nia
Kwangu kama kwako Mungu, Idhihiri pia


2. Peleleza moyo wangu, Unifunukie,
Yaliyomo ndani yangu nami niyajue.


3. Kwanza washe zako tambi. kumefunga giza;
Nijue ambavyo dhambi Ni la kuchukiza.


4. Peleleza na mawazo, Ni mbegu za mambo,
Asili ya machukizo, Maumbuo-umbo.


5. Zidi kuyapeleleza Katikati yangu,
Hata wishe Nifundisha Udhaifu wangu.


6. Hapo nikikwinamia Mbele zako, Mungu,
Hakika Nitakujua, U Mpenzi wangu.


Comments