328 NIPE MOYO WENYE SIFA

1. Nipe moyo wenye sifa Sio wa utumwa; Damu, ulionyunyizwa Wa kwimba daima.


2. Moyo msikizi, moyo Wa kunyenyekea, Moyo utawaliwao na Mwokozi pia.


3. Wenye kutubu, mnyonge, Sadiki, amini; Kamwe, kamwe, asitengwe akaaye ndani.


4. Mpya, mwema na mawazo, Mwingi wa mapenzi, Na uwe kielelezo Moyo wa Mwokozi.


5. Ni uule moyo wako; Moyo wa huruma, Yesu, natamani kwako Kukujua vyema.


6. Na ya midomo matunda Yako, nipe nami; Amani isiyokoma, Iwe yangu mimi.


7. Nitie yako tabia, Inishukie juu; Jina lako nipe pia Ndilo la pendo tu


8. Ni wa Baha utukufu; Mwana atukuke; Na Roho Mtakatifu: U Utatu pweke


Comments