331 YESU NI NURU

1. Yesu, ni nuru moyoni mwangu,
Rohoni mwangu ung'ae sana.
Giza kuu duniani,
Bwana niongoze nuruni.


2. Yesu, ni nuru moyoni mwangu,
Akufuataye hatakosa
Uwongo mwingi n-chini,
Bwana Yu Kiongozi kweli.


3. Yesu, ni nuru moyoni mwangu,
Uniongoze kwa Neno lako,
Taabu nyingi duniani,
Tangulia njiani, Bwana.


4. Watu wa Yesu, fanyeni kazi,
Tangazeni Neno lake pote,
Wengi gizani waone,
Nuru ya Bwana Yesu Kristo.


Comments