1. Ninakwenda kwetu mbinguni,
Nguvu zangu ni zake Bwana.
Simo hukumuni wala mautini,
Bwana Yesu na asifiwe.
Bwana Yesu na asifiwe, Siku zote,
njiani pote. Dhambi zangu zote
zimeondolewa, Bwana Yesu na asifiwe.
2. Ninaye adui ambaye Apenda nipotoke njia.
Mimi Sikubali, nina Kiongozi,
Bwana Yesu na asifiwe.
3. Wakihofu wengine wote, Nina nuru rohoni
Mwangu. Mbele yangu raha na furaha tele,
Bwana Yesu na asifiwe.
Comments
Post a Comment