1. Mapenzi yako yafanyike, Wewe Mfinyanzi,
Nami towe. Unifinyange upendavyo,
Mimi tayari, naja kwako.
2. Mapenzi yako yafanyike, Upeleleze
Dhambi Zote, Unisafishe vya kimwili,
Niinamapo msalabani.
3. Mapenzi yako yafanyike, Mimi dhaifu,
Mimi mnyonge. Uwezo wote, kwako kweli,
Sasa niponye, Ee, Mwokozi.
4. Mapenzi yako yafanyike, Natoa kwako vitu
Vyote. Maisha, mali, moyo, mwili,
Vyote ni vyako, kweli, kweli.
5. Mapenzi yako yafanyike, Mapenzi yangu
Yavunjike. Ninakubali uwe Bwana,
Ni mali yako, twaa kabisa.
Comments
Post a Comment