1. Mungu Mtukufu aliye Bwana,
Akamtoa Yesu Mpendwa, Mwana.
Akawa dhabihu kwa dhambi zote,
Kufungua njia kwa watu wote.
Msifuni, msifuni, Nchi imsikie.
Msifuni, msifuni Bwana mshangilie.
Njoni kwake Baba Kwa Yesu Mwana.
Mpeni heshima Aliye Bwana.
2. Ukombozi wetu, tendo la Mungu,
Ni ukamilifu kwa kila mtu.
Mwenye ukosefu akimwamini
Atasamehewa na Yesu, kweli
3. Ametufundisha mambo ya mbingu,
Tukafurahishwa na Mwana Mungu.
Ametuinua tukae naye,
Atatuongoza hata milele.
Comments
Post a Comment