Skip to main content
10 DAMU YAKO YENYE BARAKA
- Damu yako yenye baraka, Inayoosha
makosa, Ilimwagwa m-salabani, Mwokozi
ulipokufa. Nastahili ’pata hukumu,
Na siwezi mimi kujiosha. Unioshe katika
damu, Nipate kuwa safi kweli!
Safi kabisa! Safi kabisa! Unioshe katika
damu, Nipate kuwa safi kweli!
- Yesu, ulivikwa miiba, Kuangikwa juu ya
mti, Ulivumilia mateso ’jeraha na
maumivu. Ninataka kijito hicho, Niende
nisafishwe kabisa! Unioshe katika damu,
Nipate kuwa safi kweli!
- Baba, kweli nina makosa, Moyo wangu u
dhaifu; Mimi mwenye dhambi rohoni,
Nipate wokovu wapi? Yesu, kwako
m-salabani, Naja ninakuamini sasa,
Unioshe katika damu, Nipate kuwa safi kweli!
- Bwana, nimekukaribia, Nilindwe nawe
milele! Unifungue kila kamba, Uujaze
moyo wangu! Na karibu ya m-salaba,
Nitakaa hata kufa kwangu, Unioshe
katika damu, Nipate kuwa safi kweli!
Comments
Post a Comment