1. Yesu ameingia, Yu rohoni mwangu,
Amenifungulia kamba za Shetani,
Tena amenijaza Roho Mtakatifu,
Ninamsifu sasa kwa wimbo huu.
Yesu atosha kwangu, Yote ananipa,
Ameondoa dhambi, amenitakasa.
Shangwe rohoni mwangu Kama maji
mengi, Namshukuru sana Mwokozi wangu.
2. Mimi sichoki tena, naona furaha,
Njia yanipendeza Ingawa nyembamba.
Katika hali zote, Namwimbia Yesu,
Yeye Mfalme wangu, Ninamsifu!
3. Katika mwendo wangu, Ninashangilia,
Hata wakinicheka, Nikijaribiwa, Hima
Mwokozi wangu Ataninyakua toka
machoni pao, Haleluya!
Comments
Post a Comment