100 LO, BENDERA IMETWEKWA


1. Lo, bendera imetwekwa, Inapepea!
Ndugu, tusione hofu, Twende mbele tu!


Bwana Yesu atakuja, Tuwe mashujaa!
Kwa uwezo wa Mwokozi Twende kushinda!


2. Ibilisi azunguka, Atutafuta,
Anataka tuanguke, tufe, tupotee.


3. Vita kubwa, vita kali yaendelea,
Tuwe watu wenye nguvu, Twende mbele tu!


4. Basi, kwa bendera yake Twashikamana.
Atujaze nguvu zake Hata ajapo!


Comments