101 EE MLINZI TWAULIZA


1. Ee mlinzi twauliza: “Yesu yuaja lini?
Asubuhi ya Sayuni ni karibu? Twambie!”
“Msafiri angalia, Yainue macho yako.
Asubuhi ni karibu, Ee ndugu, usimame!”


2. Siku heri ya Sabato, Ya raha ni karibu.
Na dalili yake Yesu, wote wataiona.
Na rohoni tunaona, nchi nzuri ya ahadi
Asubuhi ni karibu. Ahadi zatimizwa.


3. Katika Yerusalemu, Mji mpya mbinguni,
Yesu atatumiliki, kwa pendo na Amani,
Baragumu litalia, nasi tutalisikia.
Yesu yu karibu sana kutukaribisha juu.


Comments