1. Sayuni umlaki Mfalme, Umshangilie Yesu!
Jipambe, Jiweke tayari, Kwa ajili ya arusi!
Shangwe, shangwe, Umshangilie Yesu!
Shangwe, shangwe, Umsujudie Bwana!
2. Kutoka ’tukufu wa Baba Na kiti chake
mbinguni Mwokozi alitufikia, k’azaliwa duniani.
3. Bwana alishinda mauti, Akatoka kaburini,
Akaufunua uzima, Ili tuishi milele.
4. Akawa dhabihu kamili, ’kasulibiwa mtini.
Akafa kwa ajili yetu, Tupewe wokozu wake.
5. Afika kwa wenye huzuni Kuwapa faraja yake.
Mfalme wa pendo na haki, Atamiliki milele.
Comments
Post a Comment