108 SIKU YA FURAHA


1. Siku ya Furaha imetufikia Siku nzuri
Duniani. Bwana asifiwe! Mbali na karibu,
Malaika wanamshukuru Mungu.


2. Huko Bethlehemu alipozaliwa Kristo
Bwana, Mkombozi, Pendo la Mwenyezi
Likadhihirika. Amani kwa aliowaridhia!


3. Ni karama kubwa, tuliyoipewa, Kwa mkono
Wa Baba Mungu, Roho Mfariji anatuongoza.
Atatufikisha kwake mbinguni.


Comments