109 ZIMETIMIZWA AHADI


1. Zimetimizwa ahadi njema; Amezaliwa
Mkombozi! Maneno yote ya Mungu wetu,
Aliyonena kwa manabii, Tumeyapata na
Kuyaona katika Yesu, Bwana wetu. Alitujia
Na tumepona, Twaweza kufika mbinguni.


2. Alijidhili kuwa maskini Alipofika duniani.
Tunaamini Mwokozi wetu alilazwa katika hori.
Na utukufu aliuacha Kwa Baba yake, Neema
kuu! Na twende sote horini kwake,
Tumsujudu aliye juu!


3. Mtoto huyo - mfano wetu, Ni mwanadamu, tena
Mungu. Akawa mwenye kutukomboa, Golgotha
Alitufilia. Tulipotea vibaya sana Katika dhambi
Na makosa, Kwa umaskini wa Bwana Yesu,
Twapata kuwa matajiri.


Comments