1. Asubuhi na mapema, Siku ya habari
njema, Twende sote Bethlehemu!
Mungu ameturehemu.
2. Nyota kubwa inang’aa, Pale alipo
Mwokozi. Yu Mwana pekee wa Mungu,
Mbele yake tusujudu!
3. Wachungaji wasikia Nyimbo zao malaika:
“Asifiwe Mungu juu, Duniani raha kuu!”
4. Safarini wametoka, Mariamu amechoka.
Amlaza mwana wake, Katika hori ya ng’ombe.
5. Wachungaji wanafika, Wameacha kundi lote,
Na mtoto wanamwona, Nao wamsifu Mungu.
6. Mwana yule ni Mwokozi, Msaada, Mkombozi,
Neno la kuaminiwa, Mungu ametushukia!
Comments
Post a Comment