1. Mtoto Yesu amezaliwa – Bethlehemu! Furahi watu wa Mungu, :/:Haleluya!:/:
2. Bikira alipata nafasi – Horini kumzaa. Kristo duniani. :/:Haleluya! :/:
3. Yesu ’kazaliwa pamoja na – Wanyama. Malaika ’kamwimbia. :/:Haleluya!:/:
4. Na Wachungaji wakamwabudu – Horini. Wakamsifu Bwana Yesu. :/:Haleluya!:/:
5. Twakaribishwa kuwa watoto – wa Mungu, Kukaa naye mbinguni. :/:Haleluya!:/:
6. Na sisi tumepata wokovu – Milele. Mwokozi amezaliwa. :/:Haleluya!:/:
7. Tutamwimbia kwake huko juu – Pamoja Na malaika wa Mungu. :/:Haleluya!:/:
8. Tumshukuru aliyezaliwa – Mwokozi Ndiye ndugu yetu mkuu. :/:Haleluya!:/:
Comments
Post a Comment