116 TUMWIMBIE, TUMSIFU


1. Tumwimbie, Tumsifu Yesu msalabani!
Aliteswa, alikufa, Kwa ajili ya wote.
Akashinda, ’kafufuka, ndiye Yesu Mwokozi.


2. Yesu alitukomboa, Akawa haki yetu.
Dhambi aliziondoa, Tukapata Amani.
Tutarithi utukufu, Nuru, raha na heri.


3. Yesu alipofufuka, alishinda mauti,
Akapewa mamlaka Mbinguni, duniani.
Sisi sote tumepona, Kwa kupigwa kwa Yesu.


4. Tumshukuru Mungu Baba, kwa ajili ya pendo.
Tumsifu Yesu Kristo, kwa neema yake kuu.
Tumfungulie moyo Roho Mtakatifu.


Comments