1. Nilipofika Golgotha, Niliona huko
neema kama bahari, Neema ya Mungu
Neema ya Golgotha, Ni kama bahari kuu,
Neema tele ya milele, Neema kubwa!
2. Nililemewa na dhambi Na makosa mengi
Na sikufahamu vema, Neema yake kuu.
3. Yesu alipozibeba Dhambi zangu zote,
Neema ikadhihirika, Moyo ukapona.
4. Nitakapofika kwake, Nitashangilia,
Kuimba juu ya neema, Milele mbinguni.
Comments
Post a Comment