118 YESU MWOKOZI WA AJABU


1. Yesu, Mwokozi wa ajabu Ndiye alinifilia,
Alitoa maisha yake, Kwa ’jili ya watu wote


Alikufa msalabani, Alikufa msalabani.
Kwa ’jili ya dhambi zangu zote, alikufa Msalabani.


2. Aliacha makao juu, akafika duniania.
Akateswa kwa ’jili yangu, Anifungulie njia.


3. Dhambi zangu ali’chukua, Akajitwika huzuni,
Na alijeruhiwa ili, Aniponye roho yangu.


4. Bwana Yesu alifufuka, Akapaa mbinguni juu:
Na yuaja upesi tena, Kuchukua watu wake.


Comments