119 NA’SIFU YESU KWA NGUVU


1. Na’sifu Yesu kwa nguvu yako Ulimshinda
Yule Mauti. Alidharau viumbe
Vyako, Ulimshinda msalabani.


Yesu ulimshinda Mauti, Uwezo wa Mauti
ni wapi? Kuzimu ulitoa sauti; Umepokea
mamlaka yote.


2. Huyu Mauti alichukua, Uwezo mwingi juu
ya viumbe. Wakubwa wote awapokea,
Na matajiri alioumba.


3. Kuzimu anaonea watu, Anajivuna
juu ya wote. Ulifufuka, ukaja kwetu,
Ulipobeba uwezo wote.


4. Ulipofika ukahubiri, “Nimepokea
mamlaka yote.” Tuliipenda ile habari,
Kwa kutwambia amani wote.


5. Samaha letu wa ulimwengu, Ulilitoa
kati’ mchana. Ulimwambia Baba wa mbingu:
‘Uwasamehe, wote ni wana.’


Comments