12 NIMEKOMBOLEWA NA YESU

  1. Nimekombolewa na Yesu,
    Aliyenirehemia,
    Kwa bei ya mauti yake,
    Nimekuwa mtoto wake


    Kombolewa! Nakombolewa na damu.
    Kombolewa! Mimi mwana wake kweli.



  2. Kukombolewa nafurahi,
    Kupita lugha kutamka,
    Kulionyesha pendo lake,
    Nimekuwa mtoto wake.


  3. Nitamwona, uzuri wake,
    M-falme wangu wa ’jabu.
    Na sasa najifurahisha,
    Katika neema yake.


  4. Najua taji imewekwa,
    Mbinguni tayari kwangu,
    Muda kitambo atakuja,
    Ili alipo niwepo.

Comments