1. Msalabani nilimwona Yesu, Ni Mwokozi
Aliyeniponya. Rohoni mwangu giza limetoka,
Namfuata Yesu sasa.
Sasa nimeokolewa, Na siku zote
ninaimba kwa shangwe, Na vitani
duniani, Mkombozi yupo nami.
2. Mwokozi wangu anipa nguvu, Hata nikiwa
na udhaifu. Na vita yote itakapokwisha,
Nitapata raha kwake.
3. Mwokozi wangu, ninakufuata, Raha yako
inanituliza. Na siku moja utakuja tena,
Kunichukua kwako juu.
Comments
Post a Comment