1. Msalabani Mwokozi Alizichukua dhambi. Damu iliyomwagika Ilileta ukombozi.
Ee Golgotha, Ee Golgoitha, Yesu alipojitoa! Ee Golgotha, Ee Golgotha, Hapo alinifilia!
2. Nchi ilitetemeka, Jua likatiwa giza, Mwokozi alipokufa. Kwa ’jili ya watu wote.
3. Pazia likapasuka, Kutoka juu hata chini, Sasa njia iko wazi, Ya kuingia mbinguni.
4. Ni pendo gani, Ee Yesu, Lililokufanya wewe Kutoa uhai wako Ili mimi niokoke?
Comments
Post a Comment