122 MWOKOZI KAMILI


1. Mwokozi kamili ni Bwana Yesu Aliye
Mwokozi mwema. Katika wokovu wa
Mungu mkuu Nalindwa naye kabisa.


Katika wokovu nalindwa vema, Naishi
kwa maji hai. Pendo la Mungu Linanizunguka
:/: Kunihifadhi daima :/:


2. Ninajazwa Baraka za mbinguni Kwa
Roho Mtakatifu. Nam-sifu Mwokozi
Kwa furaha, Wokovu umenijia.


3. Mwokozi mwema ndiye Bwana Yesu
Anayeondoa dhambi. Njiani aniongoza
Vizuri, Anipa nguvu ya mwendo.


4. Nitakapomwona Yesu mbinguni Baada
Ya shida huku, Nitamhimidi na kumsifu
Mwokozi wangu mpendwa.


Comments