1. Mwokozi mzuri ninaye, Zamani
sikumfahamu, Na sasa ninamshuhudia,
Wengi wapate kumwona
Wote watamwona, wote watamwona,
Mwokozi mzuri ninaye; Lo! Wote watamwona.
2. Shetani akinizuia Kum-fuata Mwokozi,
Najua Bwanangu hodari, Anayenisaidia.
3. Anapita wote kwa wema, Mfano wa Mungu,
Baba Ingawaje mimi maskini,Yeye aniita ndugu.
4. Maisha yangu namtolea, Yesu anayenipenda.
Katika ma’jabu ya Mungu, Upendo wapita yote.
Comments
Post a Comment