1. Naona pendo kubwa mno Litokalo kwa
Mwokozi, Mfano wa maji mengi yaliyomo
baharini. Linanipa tumaini Na nguvu
nyingi moyoni, Niushinde ulimwengu,
Kwa pendo kuu la Mwokozi.
Haleluya! Ni pendo kuu, Linatoka
kwa Yesu! Ee Mungu wangu,
naomba: Nijazwe pendo lako kuu!
2. Pendo hilo la ajabu, Laondoa majivuno,
Latufundisha umoja, ukweli na haki yote.
Limeleta utulivu, Tena hunipa huruma.
Tunafanyika umoja, Katika pendo la Yesu.
3. Unijaze pendo hilo, Linibidishe daima, Niwe
Najuhudi yote, Nikutumikie Bwana, Niipeleke
Injili, Kwao waliopotea! Wafahamishwe pendo
Kuu, Ulilo nalo, Ee Yesu!
Comments
Post a Comment