1. Haleluya! Nafurahi, Naimba kila siku,
Sifa kwake Yesu Kristo Aliyenikomboa.
Haleluya kwa Mwokozi, Aliyeniokoa!
Mimi wake naye wangu, Haleluya, Mwokozi!
2. Heri! Niliyeokoka Kwa neema yake kuu,
Ninapenda kumshukuru, Kwa wokovu wake
huu. Wakinung’unika wote, Mimi nijiepushe
Nitamsifu Mungu wangu leo, Hata milele.
3. Kama ndege waimbavyo Bustanini mapema,
Na sauti ya mawimbi Ivumavyo kwa nguvu,
Ndivyo nitakavyomsifu Bwana wangu kwa
shangwe. Roho yangu itaimba: Haleluya,
Mwokozi!
4. Haleluya! Furahini, Mbele za Mungu wetu!
Na watakatifu wote Mwimbieni mwokozi!
Malaika wote pia wamsifu Mwenyezi!
Mbingu zote zitajibu: “Haleluya, Amina!”
Comments
Post a Comment