126 EE MTAKATIFU MUNGU


1. Ee Mtakatifu, Mungu wa majeshi,
Leo asubuhi twaimba mbele zako!
Ee Mtakatifu, Mungu wa Rehema,
Bwana Mwenyezi, twakuabudu!


2. Ee Mtakatifu, huko juu mbinguni,
Wazee wazitupa taji mbele zako.
Jeshi la mbinguni wanakusujudu
Uliye hai hata milele.


3. Ee Mtakatifu! Utukufu wako,
Asiyetakaswa hawezi kuuona.
Wewe tu ni mwema, tunakuheshimu.
Ee Mwenye nguvu na utukufu.


4. Ee Mtakatifu! Jina lako kubwa
Lisifiwe hapa chini, na mbinguni juu!
Mungu wa neema na uwezo wote,
Mwenye baraka twakushukuru!


Comments