1. Linda roho na nafsi yangu Chini ya damu,
Ee Yesu! Makosa Na hofu zaisha, chini ya damu tu.
Chini ya damu ya Yesu, Damu yako takatifu,
Nilinde chini ya damu yako takatifu!
2. Tumaini la mwenye dhambi Chini ya damu ya Yesu,
Ukombozi kwa watu wote Chini ya damu tu.
3. Najazwa nguvu na upendo Chini ya damu ya Yesu,
Napata kuwa mtiifu Chini ya damu tu.
4. Nijazwe Roho Mtakatifu Chini ya damu,
Ee Yesu! Daima nina moyo safi,
Chini ya damu tu.
5. Ni amani moyoni mwangu Chini ya damu ya Yesu.
Karama zake nimepewa Chini ya damu tu.
Comments
Post a Comment