1. Ninapenda kumsifu Yesu Kristo, Aliyeniondoa
Dhambi zangu. Twende sote sasa tumsifu Yesu,
Kwa pendo lake la ajabu!
Haleluya Mfalme mkuu! Haleluya Mwokozi!
Na dhambi alinisamehe, Anilinda salama.
2. Baraka zake anazimimina Kama mvua
inyeshavyo juu yangu. Nastarehe mikononi
mwa Yesu, Rehema yake yanitosha.
3. Siku moja nitamwona Mwokozi Katika nchi
nzuri ya mbinguni, Nitamwona Yeye kwa
macho yangu Na sura yake ya ajabu.
Comments
Post a Comment