13 NANI AWEZA KUNIFUNGUA?

  1. Nani aweza kunifungua? Ni Bwana Yesu,
    Bwana Yesu! Kweli ushindi
    Nipate wapi? Kwa damu ya Yesu Kristo!


    Kuna nguvu ya ajabu kuu, kwa damu ya
    Yesu! Kuna nguvu ya ajabu kuu,
    Kwa damu yake Yesu!



  2. Nitawezaje kuvunja tamaa? Kwa damu
    Yake Bwana Yesu! Nikaribie kisima
    Hicho, Kisima cha damu yake!


  3. Nitawezaje kuoshwa moyo? Kwa damu
    Yake Bwana Yesu! Nitakaswe katika
    Kisima, Kisima cha damu ya yake!


  4. Nitawezaje kutenda mema? Kwa nguvu
    Yake Bwana Yesu! Nitawezaje kwenda
    Mbinguni? Kwa nguvu ya damu yake!

Comments