130 NINAPENDA KUMSIFU


1. Ninapenda kumsifu Yesu Mwokozi wangu.
Aliteswa hata kufa Ili niwekwe huru.


Mwimbieni Mkombozi Kwa upendo wake mkuu!
Alilipa deni langu, Aliniweka huru.


2. Ninapenda kushuhudu Pendo kubwa la Yesu.
Jinsi alivyoniponya, Nilipokuwa mbali


3. Ninamsifu Mkombozi, Kwa uwezo wake mkuu.
Naye anitia nguvu Ili nimshinde mwovu.


4. Ninapenda kumwimbia Yesu Kristo,
Mwokozi, Aliniokoa kweli, Niwe heri daima.


Comments