1. Mimi Mkristo nyakati zote, Hata siku ya kufa
Kwangu. Mimi Mkristo nashuhudia, Japo dunia
Inicheke. Mimi Mkristo kwa moyo wote
Ninampenda Kristo kweli, Aliyekufa kwa ’jili
Yangu, Ninastahili kumpenda.
2. Mimi Mkristo, neema kubwa, Niliokoka toka
Dhambi. Mimi Mkristo, hata ikiwa Katika shida
Duniani. Mimi Mkristo na ni askari, Napiga vita
Vya imani. Akida wangu ni Bwana Yesu,
Pamoja naye nitashinda.
3. Mimi Mkristo, na ni mgeni, Nasafiri kwenda
mbinguni. Na sitamani yaliyo huku Ninatafuta
yaliyo juu. Mimi Mkristo, na nchi yangu, Si
hapa chini ni huko juu. Hakuna njaa na shida
tena Huko wote wataridhika.
4. Mimi Mkristo, Ni neno zuri, Lanifariji moyo
wangu. Linaniondolea huzuni Napumzika kwa
Mwokozi. Mimi Mkristo maisha yote Hata nilale
kaburini. Kwa raha kubwa nitakubali
Kuchukuliwa naye Yesu
Comments
Post a Comment