1. Yesu Mwokozi, unanipenda Na pendo
Lako ni kubwa kweli. Ulinivuta karibu
Nawe, Mimi ni wako hata milele.
2. Yesu Mwokozi, unanipenda Pendo lako
Lapita akili Linanifunza kuzifahamu
Raha, upole na utu wema.
3. Yesu Mwokozi, unanipenda Mimi maskini,
Mwenye unyonge. Nimetakaswa kwa damu
Yako, Naomba unijaze upendo.
4. Yesu Mwokozi, unanipenda, Umenitilia
Wimbo mpya Wa kukusifu hata milele,
Nitakuona kama ulivyo.
Comments
Post a Comment