1. Ufurahi, moyo wangu, Umepata uheri.
:/:Sikitiko limekwisha, Yesu ni Mwokozi wangu.:/:
2. Ameponya roho yangu, Ni Mganga wa kweli,
:/:Kwa Roho Mtakatifu Abatiza watu wake.:/:
3. Yesu ameliandika, Jina langu mbinguni,
:/:Sasa mimi mali yake Milele hata milele.:/:
4. Na moyoni mwangu sasa Naimba: “Mungu Baba”.
:/:Ni furaha kubwa sana, Nina rafiki kila saa.:/:
5. Nimeondolewa dhambi, Sitarudi tena!
:/:Kweli Yesu aokoa,Wenye dhambi Kila siku.:/:
6. Nyimbo za kumsifu Mungu Zinavuma Mbinguni,
:/:Nami pia ninaimba: “Mungu Wangu usifiwe!”:/:
Comments
Post a Comment