1. Msifuni Bwana, enyi watu wake,
Kwa neema yake juu yenu! Yesu Yu
pamoja nasi atulinda, Aongoza njia yote.
Tumsifu Mungu wetu, Sababu atulinda sisi sote!
Tumsifu Mungu wetu Kwa ulinzi wake mwema!
2. Yesu alikusamehe dhambi zote.
Aponya udhaifu wako, Akufariji na
Kufuta machozi, Neema yake yakutosha
3. Anakutilia afya na uwezo wa kushinda
Katika yote. Katika mapito yake
Waongozwa Anakulinda salama.
4. Kaa ndani yake Bwana Yesu Kristo,
Ndiye mzabibu wa kweli. Hapo utaweza
Kuzaa matunda Ya kumpendeza Yesu.
5. Siku moja Bwana Yesu atakuja
Kutukaribisha mbinguni. Tutamtukuza
Yeye, Bwana wetu, Kwani alitukomboa.
6. Tunangoja siku ile, Yesu Mwokozi
atakaporudi. Tunangoja siku ile,
Sote twakuomba: “Uje!”
Comments
Post a Comment