1. Wakati wa wokovu Ulifika kweli
Yesu aliposema: “Yote yamekwisha!”
Wengi wanamjia Yesu Mkombozi,
Wapate kuokoka, Waone amani.
Mwana-Kondoo wa Mungu Twakusifu
Sana! Uzima ulitoa Kwa ajili yetu.
Umetufanya kuwa Mitume wa Mungu,
Tuhubiri Injili ya wokovu wako.
2. Kwa damu yako Yesu Ulitukomboa,
Na jua la neema Latuangazia.
Tumefahamu sasa, pendo lake Mungu,
Katika damu yako, Tumeunganishwa.
3. Njoo upesi nawe, Uliye na shaka!
Mungu atakujaza neema yake kuu.
Utapokea raha na matumaini,
Upendo wa ajabu, nguvu za kushinda.
Comments
Post a Comment