139 NINA FURAHA KUBWA


1. Nina furaha kubwa Ninapumzika,
Kwa kuwa Mungu baba Amenipokea.
Ameniweka huru Mbali na utumwa,
Na sasa ninayo raha.


2. Nilijaribu sana Kuziacha dhambi,
Lakini sikuweza Kuzishinda kweli
Sasa ninamwamini Mkombozi wangu,
Ndiye anipa ushindi.


3. Mwokozi wangu Yesu, Anayenipenda,
Alikufa mtini Kwa kuniokoa.
Nahesabiwa haki Kwa damu yake tu.
Inayonisafisha kweli.


4. Na nikijribiwa, Na mambo ya mwili,
Namkumbuka Yesu, Mshindaji kweli.
Neema inazidi Udhaifu wangu,
Namshukuru Mwokozi.


5. Na sasa Bwana Yesu Yu pamoja nami,
Neema yake kubwa Imenizunguka.
Sitasumbuka tena, Ninayo amani na
Mungu ananilinda.


6. Shetani akitaka Kunipiga vita,
Sitamwogopa kamwe Na matisho yake.
Maneno yake Mungu Yana nguvu sana
Kwa wote waaminio.


7. Ninaenenda sasa, Kwa jina la Yesu, Nitafika
Salama, Nyumbani mwa Mungu, Lakini safarini,
Naimba daima nikimshukuru Bwana.


Comments