14 MWOKOZI WANGU

  1. Mwokozi wangu ulikwenda mbinguni,
    Kuketi pamoja naye Baba. Uta’kusanya
    sisi sote huko, Mbinguni kwako
    utufikishe! Makao mema watuandalia,
    Unatungoja nyumbani kwa Baba,
    Makao mema watuandalia,
    Unatungoja nyumbani kwa Baba.


  2. Mwombezi wetu wewe, Yesu Kristo,
    Hutuombea kwa Mungu Baba.
    Unatuchunga sisi, kundi lako,
    Watusa-idia jaribuni. Na siku zote
    unatuombea, Watushindia vita kali
    huku. Na siku zote unatuombea,
    Watushindia vita kali huku.


  3. Ulipopaa uliwanyoshea, Mikono yako
    walio wako. Na hivyo siku utakaporudi,
    Ubariki wakuaminio! Ulivyokwenda
    ndivyo utarudi; Niombe, nikakeshe kwa
    imani! Ulivyokwenda ndivyo utarudi;
    Niombe, nikakeshe kwa imani!

Comments