1. Unaposumbuliwa na mashaka
Na kuogopa kwamba utashindwa,
Uhesabu baraka zake Mungu
Na utashangaa kwa wema wake.
Uhesabu baraka zote, Ulizopewa naye
Mungu! Kumbuka ulivyotendewa
Na utashangaa kwa wema wake!
2. Ukiudhiwa na huzuni nyingi,
Ukiona msalaba ni mzito,
Uhesabu baraka ziku zote
Kwa moyo wote utamsifu Mungu.
3. Wengi watamani mali ya huku,
Utajiri wako ni Bwana Yesu.
Hesabu baraka na ukumbuke:
Mali haiwezi kukuokoa.
4. Katika mambo yote duniani,
Ukumbuke pendo kubwa la Mungu.
Na ujumlishe baraka zote,
Mwisho utachukuliwa kwake juu.
Comments
Post a Comment