141 KWA BWANA YESU TWAPATA


1. Kwa Bwana Yesu twapata Furaha na shangwe.
Anatuongoza vema, Anatushibisha.
Yeye yupo pamoja nasi, Neema yake yatutosha.
Haleluya, Haleluya,Haleluya , Bwana!


2. Ni vema kumpenda Yesu, Mkombozi wetu.
Tukimfuata yeye Hatutapotea.
Furaha yetu itabaki, Hata vyote vingetoweka.
Haleluya, Haleleluya, Haleluya, Bwana!


3. Hata liwepo giza kuu, Jua likifichwa,
Na tunapojaribiwa Ni kwa kitambo tu.
Mbinguni hatutayaona Majaribu wala huzuni.
Heleluya, Haleluya, Haleluya, Bwana!


4. Tusisumbukie tena Chakula na nyumba,
Kwani vyote twavipata, Kwa neema ya Mungu.
Njiani anatuongoza, Aibeba mizigo yetu.
Haleluya, Haleluya, Haleluya Bwana!


5. Ikiwa ni vyema huku Kumwamini Yesu,
Furaha gani huko juu, Kuonana naye!
Tutashangilia milele, Utukufu hautaisha.
Haleluya, Haleluya, Haleluya, Bwana!


Comments