1. Yesu ni furaha yangu, Amejaa upendo,
Naye anamwimarisha, Aliye mdhaifu.
Ananipa ujasiri, na nguvu ya kushinda.
Hata nitakapokufa, Sitakuwa na hofu.
2. Nimeungwa na Mwokozi, Katika pendo lake.
Hata kifo hakiwezi Kunitenga na Yesu.
Mimi wake siku zote, Ninapenda kumtii.
Kwa neema nimepona, Nisiishi dhambini.
3. Kwa mikono ya upendo, Nakumbatiwa naye.
Sitaweza kueleza, Upendo wake kwangu.
Napokea nguzu zake, Zinanijaza moyo.
Katika safari yangu Yesu ananiongoza
Comments
Post a Comment