143 HERI HAKIKA NA FURAHA


1. Heri hakika na furaha, Yesu ni wangu
nami wake. Moyoni mwangu ni salama,
Nimeokoka haleluya!


Yesu ni wangu, Asifiwe! Nitamwimbia
siku zote. Na nitamwona mbinguni juu,
Moyoni mwangu furaha kuu.


2. Nilijitoa kwake Yesu, Nikapewa wokovu
mkuu. Mbinguni wote hufurahi,
Anapotubu mwenye dhambi.


3. Sasa nina-msifu Yesu, Nashibishwa
rohoni mwangu. Mimi si kitu mbele zake,
Nimeokoka kwa neema.


4. Nimepokea ubatizo, katika Roho
Mtakatifu. Moto unawaka moyoni,
Mimi shahidi wake Yesu.


Comments