1. Upendo wa Bwana Yesu, Ni wa ajabu kweli,
Wafanana na chemchemi Inayobubujika.
Yesu amelifungua Lango la mbinguni juu,
Ili niingie humo, Kwa neema yake kuu.
2. Kama ndege mtegoni, Ndivyo nilivyonaswa,
Nikamlilia Yesu Naye akaniponya.
3. Ni ajabu kubwa kweli, Dhambi alizifuta,
Juu ya Rehema yake, Naimba kwa furaha.
4. Siku nitakapofika, Kwa lango la mbinguni,
Nitaweza kuingia, Kwa pendo la Mwokozi.
Comments
Post a Comment