146 NINAYE MUNGU WA AJABU


1. Ninaye Mungu wa ajabu kuu, Anishauri,
Anifariji, katika giza, Ananiangaza,
Yeye ndiye tumaini langu la kweli.


Mungu wetu yu mwema, atupenda
daima, Akamtuma Mwokozi, Atuoke
dhambini.


2. Nikizikuta dhiki na shida, Kwa Baba Yangu
Mungu wa mbingu Ninayo raha Niko salama,
hata nikikuta mawimbi Safarini.


3. Nikiwa mbali Toka nyumbani, sihofu
Tena Nipo na Bwana, Ananishika Namsikia
Yumo chomboni na kutuliza mawimbi.


4. Hata mwishoni Mwa safarini, Nikiamini
nina amani. Hata nikifa Nitafufuka.
Nitasimama na kuimba wimbo mpya.


Comments