1. Mwenyezi Mungu wa nyakati zote
Ni kimbilio la watu wote. Katika vita
anawashindia, Na kuwaokoa watu wake.
Mfalme mkubwa ndiye Mungu, Vitani
atushindia. Kwa shangwe kuu tunamsifu,
Tumwimbie Mungu wetu!
2. Mwenyezi Mungu wa nyakati zote
Aliwaokoa utumwani, Na wakafikishwa
ng’ambo salama, Kwa njia kavu kati’ bahari.
3. Mwenyezi Mungu wa nyakati zote
Alimshinda Baali Karmeli. Akasikia ombi
la Eliya, Moto wa mbinguni ukashuka.
4. Mwenyezi Mungu wa nyakati zote
Akawa na Daudi vitani; Daudi alitupa jiwe
lake, Na Yule Goliati akafa.
5. Mwenyezi Mungu wa nyakati zote
Uovu wote washindwa naye. Atamseta
Yule mdanganyi, Shetani chini ya miguu yake.
6. Mwenyezi Mungu wa nyakati zote
Atuongoza kwa neno lake. Anatulinda
Hatarini huku, Mbinguni tutafika salama.
Comments
Post a Comment