1. Nguvu za Mungu ziliwashukia Wanafunzi wote
siku ya Pentekoste kule Yerusalemu. Nguvu
hiyo ya Mwokozi, Ni sawa kama zamani!
Nguvu zake, Nguvu zake Mungu
Hazibadiliki, hazibadiliki! Nguvu zake,
Nguvu zake Mungu, Hazibadiliki
2. Bwana Yesu aliwapa ahadi: “Mtapata nguvu!”
Roho wake akashuka. Wakamsifu Mungu.
Waliokuwa dhaifu Wakahubiri kwa nguvu.
3. Roho Mtakatifu aingiapo Hututia nguvu,
Ili tupate imani Ya kumshinda mwovu.
Kwa moyo unaowaka, Tuite watu kwa Yesu!
4. Roho uingie moyoni mwangu, Washa
moto wako, Nipate kusimama imara
siku zote! Uje tena hapa kwetu,
Kama siku za mitume!
Comments
Post a Comment